Tafsiri ya Sura Muhammad 47:38
﴿هَا أَنتُمْ هَٰؤُلَاءِ تُدْعَوْنَ لِتُنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَمِنكُم مَّن يَبْخَلُ وَمَن يَبْخَلْ فَإِنَّمَا يَبْخَلُ عَن نَّفْسِهِ وَاللَّهُ الْغَنِيُّ وَأَنتُمُ الْفُقَرَاءُ وَإِن تَتَوَلَّوْا يَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوا أَمْثَالَكُم﴾
Tafsiri ya maana
Angalieni! Nyinyi mnaitwa mtumie katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wapo katika nyinyi wanao fanya ubakhili. Na anaye fanya ubakhili basi anajifanyia ubakhili mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu si mhitaji, na nyinyi ndio wahitaji. Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani — v1.0.1 · QuranEnc.comManeno ya maimamu wawili yametolewa kwa Kiarabu asilia, neno kwa neno, pamoja na marejeo.
Imam Ibn al-Qayyim
يذهب بهم ويأتي بأطوع واتقى له منهم في الدنيا وذلك قوله {وإن تتولوا يستبدل قوما غيركم ثم لا يكونوا أمثالكم} يعني بل يكونوا خيرا منكم«التبيان في أقسام القرآن» 1/197